Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (MKUMBI)

Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (MKUMBI)

Mazingira ya Biashara na Uwekezaji ni muhimu katika Taifa lolote,  ili Taifa litambulike kuwa lina mazingira bora ya uwekezaji na  ufanyaji biashara lazima kuwepo na sera bora, sheria, taratibu, kanuni, na mifumo ya Tehama ambayo itawezesha sekta binafsi kustawi. Kila Taifa Duniani linapambana kuwa na mzaingira ya biashara na uwekezaji bora. Kama ilivyo katika mataifa mengine uboreshaji wa maz...

Malengo

  1. Kuanzisha na kutekeleza shughuli za kuhamasisha na kuhakikisha taratibu bora za udhibiti, utoaji leseni na vibali

  2. Kuhakikisha majukumu ya mamlaka za udhibiti yanayoingiliana yanaondolewa na yanayofanana yanaunganishwa

  3. Kukuza uwazi katika mamlaka za udhibiti kwa kuweka mifumo ya TEHAMA inayotoa taarifa, huduma na taratibu zinazohitajika kwa umma kwa wakati

  4. Kuanzisha mfumo madhubuti wa ufuatiliaji na tathimini ili kuhakikisha utekelezaji mzuri wa maboresho yanayopendekezwa

Sera & Mikakati

UTEKELEZAJI

  • star
  • star
  • star
  • star
  • star
  • Misingi 10 ya Maboresho ya MKUMBI

    i) Maboresho yanayofanywa na mamlaka za udhibiti yasilenge kuongeza mapato bali kukidhi gharama za utoaji huduma.

    ii) Sheria, Kanuni na Taratibu zilenge kutekeleza sera ya biashara, ushindani, kumlinda mlaji na huduma za umma.

    iii) Kukuza ushindani wa kimkakati wenye usawa, tija na ubunifu kwa kupunguza tozo na ada.

    iv) Majukumu ya mamlaka za udhibiti yanayoingiliana yaondolewa na yanayofanana yaunganishwe.

    v) Ukusanyaji wa mapato utumie nyezo rahisi na rafiki kwa kutumia mifumo ya dirisha moja na vituo vya pamoja.

    vi) Udhibiti uwe kwa lengo la kuendeleza sekta husika au uzalishaji.

    vii) Kuwa na mifumo ya udhibiti yenye uhakika, endelevu na inayotabirika.

    viii) Kuhakikisha kuwa maboresho ya kupunguza kanuni hayaondoi mamlaka ya udhibiti.

    ix) Kanuni zote zitakazotungwa zifanyiwe tathmini ya athari ya udhibiti kabla ya kuidhinishwa kutumika.

    x) Chagamoto za kiutendaji ndani na baina ya mamlaka za udhibiti zitatuliwe.

    Tazama Video

    Wasiliana Nasi

    • Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji
    • Mji wa Serikali-Mtumba 1 Barabara ya Ardhi, S.L.P. 104, 40403 DODOMA.
    • +255 (026) 2962384
    • ps@planninginvestment.go.tz