Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dk. Tausi Kida (wa pili kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Eliakim Maswi (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Stephen Mbundi (katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Bw. Elijah Mwandubya (wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili na kuzungumza kabla ya kikao cha Makatibu Wakuu cha maandalizi ya Mkutano wa 46 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambacho kinatarajiwa kufanyika tarehe 28 Novemba, 2024 katika ukumbi wa Makao Makuu ya Afrika Mashariki, jijini Arusha.