Habari
KILA MTANZANIA ANATAKIWA KUSHIRIKI UTEKELEZAJI WA DIRA 2050
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt.Pius Chaya amesema ili kufikia malengo yaliyopo kwenye Dira 2050 ikiwemo kufikia uchumi wa Dola za Marekani Trilioni Moja ni muhimu kwa kila Mtanzania kushiriki katika utekelezaji wake.
Akizungumza kama mtoa Mada mkuu kwenye Mhadhara ulioandaliwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Dodoma, kuhusu Nafasi ya Mipango ya Maendeleo Vijijini katika utekelezaji wa Dira 2050, Dkt.Chaya amesema kila Mtanzania ana nafasi muhimu ya kutekeleza kwa vitendo yaliyomo kwenye Dira mpaka kwenye ngazi za vijiji.
”serikali kupitia Tume ya Taifa ya Mipango imejipanga ipasavyo katika kuhakikisha utekelezaji wa Dira 2050 unafanyika Kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kufanya tathimini ya kila hatua” amesema Dkt. Chaya
Kwa upande mwingine ametoa wito kwa wanataaluma kufanya tafiti ambazo matokeo yake yatajibu kero za Wananchi badala ya kuyaacha kwenye makabati ili kufikia Dira 2050.
