Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

PROF. MKUMBO AWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA MWAKA 2025/26 NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2026/27


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo (Mb.), amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/26 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2026/27 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Bungeni Jijini Dodoma.

Katika wasilisho hilo, Mheshimiwa Waziri aliwasilisha mafungu matatu ambayo ni Fungu la 011 (Wizara), Fungu la 007 (Msajili wa Hazina) na Fungu la 066 (Tume ya Taifa ya Mipango).