Habari
SERIKALI IMELIHAKIKISHIA BUNGE KUWA IKO TAYARI KUTEKELEZA SHUGHULI ZAKE KWA NAMNA ISIYO YA KAWAIDA (BUSINESS UNUSUAL), ILI KUHAKIKISHA NCHI INAFIKIA UCHUMI WA DOLA ZA MAREKANI TRILION 1 KAMA ILIVYO AINISHWA KATIKA DIRA 2050.
Serikali imelihakikishia Bunge kuwa iko tayari kutekeleza shughuli zake kwa namna isiyo ya kawaida (business unusual), ili kuhakikisha nchi inafikia Uchumi wa dola za Marekani Trilion 1 kama ilivyo ainishwa katika Dira 2050.
Hatua hiyo, ni maamuzi ya Serikali chini Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na imewekwa wazi na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo.
Waziri Mkumbo amesema hayo, akihutubia Bunge wakati wa kuhitimisha mjadala kuhusu Nyenzo za utekelezaji wa Dira 2050 ambazo ni Mpango Elekezi wa Maendeleo wa Muda Mrefu 2026/27–2050/51, Mapendekezo ya Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2026/27–2030/31 na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2026/27.
