Habari
TANZANIA NA URUSI KUIMARISHA USHIRIKIANO WA BIASHARA NA UWEKEZAJI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, akitoa Hotuba fupi katika Jukwa la Pamoja la Biashara na Uwekezaji lililoandaliwa na Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi(TISEZA), katika ukumbi wa AICC, jijjni Arusha.
Jukwaa hilo ni mwendelezo wa Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja kati ya Tanzania na Urusi katika masuala ya biashara na Uwekezaji ulioanza Jumanne iliyopita ukiwakutanisha watalaamu mbalimbali kutoka katika nchi hizo mbili.
Katika hutuba yake, Prof. Mkumbo alisema Tanzania na Urusi ni nchi marafiki wa siku nyingi ambapo uhusiano na ushirikiano umedumu kwa zaidi ya miaka 60, hivyo ushirikiano huo utachochea ukuaji wa biashara katika nchi hizo mbili.
Jukwaa hilo, limehudhuriwa na Waziri wa Maendeleo ya Uchumi wa Shirikisho la Urusi, Maksim Reshetnikov ambaye ameongoza ujumbe mkubwa kutoka Urusi kutoka sekta mbalimbali.
Akizungumza katika Jukwaa hilo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alisema ili kudhibitisha ushirikiano kati ya Urusi na Tanzania, Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), itaanza safari kwenda Urusi ambapo inatarajiwa itaongeza chachu ya biashara baina ya hizo nchi mbili.
