Habari
TANZANIA NA WORLD GOLD COUNCIL KUONGEZA THAMANI DHAHABU
Serikali ya Tanzania imepiga hatua nyingine katika kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha wananchi wake kwa vitendo.
Leo, Februari 13, 2026, Mawaziri wa kisekta wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, wamefanya mazungumzo ya kimkakati na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Dhahabu Duniani (WGC), Bw. David Tait.
Baadhi ya Mambo makuu yaliyojiri katika mazungumzo hayo ni pamoja na;
i. Uongezaji Thamani (Value Addition): Kusisitiza sera ya kutokubali kusafirisha dhahabu ghafi nje ya nchi. Lengo ni kuvutia uwekezaji wa viwanda vya kusafisha na kutengeneza bidhaa za dhahabu hapa nchini.
ii. Urasimishaji wa Wachimbaji Wadogo: Mpango wa kuwawezesha wachimbaji wadogo (ambao wanachangia 40% ya uzalishaji) kufanya kazi kwa tija na kuzingatia mazingira.
iii. Ushirikiano wa Kimataifa: WGC imevutiwa na mfumo wa Tanzania na kuichagua kuipa ushirikiano wa kukuza sekta ya madini, kwa kuwajengea uwezo, maarifa na teknolojia wachikmbaji wadogo ili iwe kitovu (hub) cha mfano wa namna ya kukuza sekta ya dhahabu.
Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Maendeleo ya Vijana Mhe. Joel Nanauka na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dorothy Gwajima wameshiriki katika mazungumzo hayo.
