Habari
TANZANIA YAIMARISHA UHUSIANO WA KIUWEKEZAJI NA AB INBEV NA TBL
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb), Januari 19, alikutana na kufanya mazungumzo ya uwili na wawakilishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) pamoja na kampuni mama ya AB InBev katika Mji wa Davos-Klosters, Uswisi.
Katika mazungumzo hayo, Prof. Mkumbo amesisitiza dhamira ya Tanzania ya kuendelea kuweka mazingira ya biashara bora ya uwekezaji na biashara, yanayotabirika, na rafiki kwa uwekezaji.
Mhe. Waziri, aliitaja AB InBev na TBL kama washirika muhimu wa kimkakati wa muda mrefu katika ajenda ya maendeleo ya nchi.
Vilevile, Waziri alisisitiza nia ya Serikali ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuona zao la shayiri (barley) na malighafi nyingine muhimu zikizalishwa hapa nchini.
Hatua hiyo, inalenga kuimarisha mnyororo wa thamani kwa kuwaunganisha wakulima na soko ili kuhakikisha wananufaika na shughuli za wawekezaji hao.
