Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

WAZIRI MKUMBO AZINDUA DIRISHA LA IMBEJU, AHIMIZA VIJANA KUCHANGAMKIA MITAJI NA MAFUNZO


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb), amepongeza program ya Go Green na Imbeju kwa kuanza kutekeleza wito wa Mheshimiwa Rais wa kuhakikisha kuwa Sekta ya umma na Sekta binafsi zinaoanishe mipango yake na malengo ya Dira 2050.

Waziri Mkumbo, ametoa pongezi hizo leo alipofungua dirisha la uwezeshaji vijana chini ya mpango wa CRDB Foundation “Go Green na IMBEJU” unaolenga kupanda mbegu kwa vijana kwa kutoa mafunzo, mitaji na malezi.

“uamuzi wa CRDB Foundation kuanzisha programu hii ni uamuzi wa maana sana na ni mchango makini kwa nchi yetu katika kurasimisha shughuli za kiuchumi na kuwaondoa watanzania, hususan vijana na wanawake, katika umaskini” alisema Prof. Mkumbo.

Aidha, Mheshimiwa Waziri alieza kuwa hatua ya Benki hiyo kuanzisha Programu ya Go Green iMbeju, ni utekelezaji wa Nguzo ya Tatu ya Dira 2050 inayolenga kulinda na kutunza mazingira na kuwa na matumizi endelevu ya raslimali kwa faida ya kizazi cha leo na vizazi vijavyo.

Programu hiyo, inaandaa fursa ambazo ni nyenzo muhimu na suluhisho endelevu kwa vijana katika Kuchochea ushiriki wa vijana katika uchumi wa kijani, Kuwezesha biashara changa, ndogo na za kati zinazomilikiwa na vijana.

Vile vile, Kukuza biashara bunifu za vijana na kuwaunganisha na masoko ya kimataifa, Kutengeza ajira na kuwandaa vijana na uchumi wa kidigitali, Kuchochea matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira

Mheshimiwa Waziri amewahakikishia vijana kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira sahihi ya biashara na uwekezaji ili kuunga mkono na kuwezesha biashara na uwekezaji nchini.