Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.) wa pili (kushoto), Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo (Mb) wa kwanza (kushoto), Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida wa pili (kulia), na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Dkt. Fred Msemwa wa kwanza (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasilishwa Bungeni Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2025/26. Kikao hicho kimefanyika tarehe 11 Machi, 2024 Mkoani Dodoma.