Habari
DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 YAWASILISHWA BUNGENI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mheshimiwa Profesa Kitila Mkumbo (katikati), Naibu Waziri, Stanslaus Nyongo (kulia kwake), Katibu Mkuu, Dkt. Tausi Kida (kushoto kwake), na Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Fred Msemwa (wa pili kutoka kulia) wengine ni Dkt. Linda Ezekiel, Naibu Katibu Mtendaji Menejimenti ya Utendaji na Tathmini (wa mwisho kushoto kwake na Dkt. Mursali Milanzi (Naibu Katibu Mtendaji-Mipango ya Kitaifa (wa mwisho kulia) pamoja na viongozi mbalimbali wa Tume ya Mipango.
Picha hii imepigwa leo katika lango la Ukumbi wa Bunge ikiwa ni ishara ya kukamilisha zoezi la kuwasilisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 Bungeni lililofanywa na Mheshimiwa Profesa Kitila Mkumbo mapema asubuhi.
Dira hiyo mpya inayotarajiwa kutoa mwelekeo wa maendeleo ya taifa kwa karibu miongo mitatu ijayo ina shabaha ya kujenga Uchumi wa kati ngazi ya juu wenye pato la Taifa la dola trioni moja huku pato la mtu mmoja mmoja likikatarajiwa kufikia dola 7,000 ifikapo 2050.
Aidha, baada ya kukabidhiwa Bungeni, Dira hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 17 Julai, 2025.