Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

DIRA YA TAIFA 2050 KUPELEKWA BUNGENI KWA KUIDHINISHWA


DODOMA – Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 inatarajiwa kuwasilishwa Bungeni Juni 26, 2025, kwa ajili ya kuidhinishwa na wabunge kabla ya kuzinduliwa rasmi na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida leo Juni 19, jijini Dodoma alipotembelea maonesho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park.

Dkt. Kida, alisisitiza kuwa Dira hiyo itaambatana na mpango wa muda mrefu wa utekelezaji wa maono yaliyomo ndani yake.

Katika ziara yake, Dkt. Kida pia alitembelea mabanda ya Taasisi zilizo chini ya Ofisi yake, ikiwemo banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Kiuchumi (EPZA), kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na taasisi hizo.