Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

Dkt. Kida ahudhuria Mkutano wa Mawaziri wa Fedha, Mipango na Maendeleo ya kiuchumi nchini Zimbabwe.


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida amemwakilisha Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, katika Mkutano wa Mawaziri wa Fedha, Mipango na Maendeleo ya kiuchumi unaofanyika leo Machi 4-5, 2024, katika Hotel ya Water Falls nchini Zimbabwe.

Mkutano huo ulitanguliwa na Mkutano wa 42 wa Wataalamu uliofanyika Februari 28 hadi Machi 1, 2024, ambapo Dkt. Kida alipata fursa ya kushiriki na kuchangia mada mbalimbali zikiwemo za Maendeleo ya Uchumi  na kijamii yanayotokea katika bara la Afrika.

(Pichani Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida na balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Mhe. Simon Sirro)