Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

DKT. KIDA AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA (EACLC) ULIOPO UBUNGO


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida Machi 18, 2024 ametembelea mradi wa uwekezaji wa East African Commercial and Logistics Center (EACLC) uliopo Ubungo Jijini Dar es Salaam na kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi huo. 

Uwekezaji unaofanyika katika mradi huo uliopo Manispaa ya Ubungo una thamani ya dola za kimarekani milioni 110 na ni miongoni mwa miradi iliyosajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ujenzi wa mradi huo unahusisha ujenzi wa Kituo kikubwa cha biashara kitakachojumuisha maduka na ofisi 2000 na ulianza kujengwa April, 2023 ukitarajiwa kukamilika Julai 2024.

Dkt. Kida ametembelea eneo hilo na kujionea hatua zilizofikia na kupata maelezo ya kitaalam kuhusu namna mradi utakavyofanya kazi mara baada ya kukamilika.