Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

DKT. KIDA AKUTANA NA MWENYEKITI WA BODI WA KAMPUNI YA HUAWEI TANZANIA


Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida, leo amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Kampuni ya Huawei Tanzania, Bw. Jason Yi, jijini Dodoma.

Mazungumzo hayo yanaashiria hatua kubwa kwa mustakabali wa maendeleo ya teknolojia nchini.

Katika kikao hicho, Dkt. Kida na Bw. Yi walijadili kwa kina masuala ya teknolojia, hususani namna ya kuboresha ushirikiano kati ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji na Huawei Tanzania.

Mazungumzo haya yameweka msingi wa mipango mipya na kuimarisha ushirikiano wa kiufanisi katika teknolojia, ili kufanikisha malengo ya maendeleo ya kidijitali nchini.

Dkt. Kida amesisitiza kuwa serikali inajizatiti kuimarisha mazingira ya uwekezaji, kwa kuweka mipango shirikishi itakayochochea ukuaji wa sekta binafsi.

“Tanzania itaendelea kuwa mshirika madhubuti kwa wawekezaji wa ndani na nje, ili kuwezesha sekta binafsi kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi,” amesema Katibu Mkuu.