Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

DKT. MSEMWA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA ANTON KAZMIN MKURUGENZI MTENDAJI WA LIFEDX AFRICA CO. LTD


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Uwekezaji, Dkt. Fred Msemwa, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Anton Kazmin (Kulia)ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa LifeDX Africa Co. Ltd, kampuni ya teknolojia ya kibayolojia inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa tiba vya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali.

Mazungumzo hayo yalilenga namna na kuboresha masuala ya uwekezaji katika sekta ya afya. Kampuni ya Life DX iliyopo Dar es Salaam, inaendesha shughuli za utafiti, maendeleo, na uzalishaji wa vipimo vya haraka vya maabara.

Kampuni hiyo inajikita katika kuboresha upatikanaji wa vipimo vya afya kupitia maeneo yafuatayo:-Utengenezaji wa vipimo vya haraka, vipimo vya teknolojia ya Lateral Flow na ELISA kwa ajili ya kugundua magonjwa mbalimbali kama malaria, VVU (HIV), kifua kikuu (TB), homa ya ini, magonjwa ya zinaa (STIs), na magonjwa ya kitropiki.