Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

MHE. NDEJEMBI: UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MADINI NI CHACHU YA KUFIKIA MALENGO YA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Pancras Ndejembi, amefungua Kongamano la Saba la Madini na Uwekezaji jijini Dar es Salaam.

Akifungua kongamano hilo, Mhe. Ndejembi amesisitiza umuhimu wa sekta ya madini katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kuifikisha Tanzania katika uchumi wa dola za Marekani trilioni moja.

Kongamano hilo limehudhuriwa pia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, aliyeungana na viongozi wengine wa Serikali kujadili mchango wa sekta ya madini katika kukuza uchumi na maendeleo ya taifa.

Viongozi wengine waliohudhuria ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Mipango, Dkt. Tausi Kida, ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), pamoja na Katibu Mkuu wa Uwekezaji, Dkt. Fred Msemwa.

Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, kupitia Tume ya Taifa ya Mipango (NPC), ndiyo iliyoandaa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na ina jukumu la kuratibu utekelezaji wake ili kufikia malengo ya kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kipato cha kati ngazi ya juu.