Habari
DKT. TAUSI KIDA AKUTANA NA BALOZI WA UMOJA WA ULAYA (EU) BI. CATHERINE GAU.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida Machi 15, 2024 amefanya mazungumzo na Mhe. Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Bi. Catherine Gau jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine wawili hao wamejadili kuhusu namna ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano hususani katika eneo la Uwekezaji na Mipango ya maendeleo ya kitaifa.
EU ni Mshirika muhimu wa Serikali katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo msaada wa zaidi ya Shillingi bilioni 60 kusaidia kuboresha mazingira ya biashara nchini.