Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

Serikali Kuhuisha Sera ya Uwekezaji.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema kuwa Serikali kupitia Ofisi yake ipo katika mchakato wa kuhuisha Sera ya Uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wengi nchini.

Prof. Mkumbo amesema hayo leo Februari 6, 2023 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Esther Malleko aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kubadili Sera ya Uwekezaji iliyopitwa na wakati ili kuvutia wawekezaji nchini.

"Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji ipo katika mchakato wa kuhuisha Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya mwaka 1996 ili iendane na mazingira ya sasa. Tayari rasimu ya sera mpya na mkakati wa utekelezaji imeshaandaliwa na sasa itaingizwa katika mchakato wa maamuzi ndani ya Serikali", amesema Prof. Mkumbo.