Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

KAMPUNI YA UNITED GREEN YA UINGEREZA KUFANYA UWEKEZAJI MKUBWA NA WA KIMKAKATI KWENYE SEKTA YA KILIMO NA MIFUGO.


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida amepokea mapendekezo ya Kampuni ya United Green ya nchini Uingereza yenye nia ya kufanya uwekezaji mkubwa wa kimkakati kwenye sekta za Kilimo na Mifugo wenye thamani ya Dola za marekani million 365.

Katibu Mkuu ameikaribisha kampuni hiyo kuufanya mradi huo nchini Tanzania na kuongezea kuwa wazo dhana (Concept Note) ya kampuni hiyo kuhusu mawanda ya mradi husika unaakisi Mipango mbalimbali muhimu ya Serikali.

Aidha, Dkt. Kida amewaeleza kuwa Serikali itapitia pendekezo hilo na kuwashauri zaidi namna ya kushirikiana na sekta ya Umma na sekta binafsi kutumiza azma yao ya kuwekeza hapa nchini.

Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 25 Oktoba 2023 katika ofisi za TIC, Golden Jubilee Tower Jijini Dar es Salaam na kimehudhuriwa na Wizara ya Fedha, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, TADB, Ofisi ya Msajili wa Hazina na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).