Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

KATIBU MKUU, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI AFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI CHINA


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida amefanya ziara ya kikazi katika Jamhuri ya Watu wa China tarehe 04 Septemba, 2023 na kukutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wawekezaji wakubwa nchini China kutoka Majimbo ya Hunan na Shandong.
 
Mkutano huo umeandaliwa na Ofisi ya Ubalozi wa China kwa kushirikiana na Chemba za Wafanyabiashara wa Shandong na Hunan, ambapo Katibu Mkuu Dkt. Kida ameelezea fursa zilizopo nchini Tanzania pamoja na utekelezaji wa mikakati ya maboresho ya mazingira ya uwekezaji nchini.
 
Wawekezaji hao wameonesha nia ya kuwekeza katika viwanda vya kuzalisha kemikali, sekta ya usafirishaji, nishati, bidhaa za ngozi, nyumba za biashara, ujenzi na hospitali.
 
Vilevile, Katibu Mkuu Dkt. Kida amepata fursa ya kufanya mazungumzo na Bw. Yiming Xu, Mwenyekiti wa Makampuni ya DA YA Group ambao tayari wanatekeleza mradi wa uwekezaji wa Tanzania Safaris ambao unajumuisha ujenzi wa hoteli, kambi za watalii na viwanja vya golf jijini Arusha, Serengeti na Zanzibar.