Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO ATOA MAONI YAKE KUHUSU DIRA YA MAENDELEO YA TAIFA 2050


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ametoa maoni yake kuhusu Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ambapo anatamani Dira hiyo iakisi matamaniao ya wananchi naTanzania waitakayo 2050.

Dkt. Mpango ametoa maoni yake kwa Timu Kuu ya Uandishi wa Dira Oktoba 30, Chamwino, Dodoma, iliyongonzwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb), Naibu Waziri wa Nchi, Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo (Mb) na Katibu Mkuu Dkt. Tausi Mbaga Kida.

Aidha, Mhe. Dkt. Mpango amesisitiza kuwa, katika Rasimu ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 angependa kuona Taifa la Haki na Uwajibikaji.


Mchakato wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 unaendelea ambapo hadi kufikia sasa ipo Rasimu ya kwanza, na viongozi mbalimbali wa ngazi ya juu ya kitaifa wanaendelea kukutana na Timu kuu ya Uandishi wa Dira na kutoa maoni yao.