Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

MHE. NYONGO AWAALIKA WAWEKEZAJI KUTOKA INDIA KUJA TANZANIA KUWEKEZA KATIKA SEKTA MBALIMBALI


Serikali ya Tanzania imewaalika wawekezaji kutoka India, ikiwataka kushiriki katika shughuli za uwekezaji nchini kwenye sekta mbalimbali za kiuchumi ikiwemo ujenzi na ukarabati wa miundombinu, kilimo na viwanda ili kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb.), katika hotuba yake kwenye mkutano wa kibiashara baina ya India na Afrika unaofanyika New Delhi, India, ambapo amefafanua fursa za uwekezaji zinavyofungua milango mipya ya kiuchumi katika sekta mbalimbali nchini.

“Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ninawakaribisha kushirikiana nasi katika juhudi za kuimarisha uchumi wa nchi yetu. Ninawahakikisha kuwa Tanzania imeweka mazingira bora kwa uwekezaji, ikijumuisha motisha mbalimbali, iwe unatekeleza mradi peke yako au kwa kushirikiana na Serikali" Amesema.