Habari
MHE. NYONGO AWASISITIZA WENYEVITI NA WATENDAJI WAKUU WA MASHIRIKA KUSIMAMIA MAGEUZI KATIKA KUCHOCHEA UKUAJI WA UCHUMI
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanslaus Nyongo amewasisitiza wenyeviti na Watendaji Wakuu wa Taasisi kuendelea kusimamia mageuzi kwa karibu, ili mashirika yaendelee kuchangia kikamilifu katika uchumi wa Taifa
Mhe. Nyongo amesema hatua hiyo ni nyenzo muhimu ya kufanikisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ambayo inalenga kuifikisha Tanzania katika uchumi wenye thamani ya Dola za Kimarekani Trilioni 1.
Mhe. Nyongo ametoa wito huo wakati akihutubia washiriki wa Kikao Kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma (CEO’s Forum 2025 kilichofanyika Mkoani Arusha mapema leo.
Aidha, ameongeza kuwa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji itaendelea kuhakikisha maazimio yaliyowekwa na kikao kazi yanatekelezwa kikamilifu.
