Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

MM Connect Africa kukuza Uwekezaji nchini Tanzania.


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt.Tausi kida ameshiriki kikao cha majadiliano juu ya majukumu mbalimbali yanayofanywa na MM Connect Africa hususani upande wa kukuza Uwekezaji nchini Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla.
 
kikao hicho kilichofanyika tarehe 30 Oktoba, 2023  katika ofisi za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimehudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa (TIC) Bw. Giliad Teri pamoja na Mwanzilishi wa MM Connect Africa, Bi. Mwamvita Makamba.