Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI NA GATSBY AFRICA WAJADILI KUIMARISHA USHIRIKIANO


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Gatsby Africa-Tanzania, Bw. Samweli Kilua, jijini Dodoma.

Mazungumzo yao yamehusu kuimarisha ushirikiano katika kubuni, kujengeana uwezo, na kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa.

Aidha, viongozi hao wamegusia masuala ya uwekezaji na maboresho ya mazingira ya ufanyaji biashara nchini, hususani utekelezaji wa mikakati inayolenga kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.