Habari
OR-MU KUWAHAKIKISHIA USHIRIKIANO WAWEKEZAJI NA WADAU WOTE WA SEKTA BINAFSI
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Pius S. Chaya (Mb.), akitoa neno la ukaribisho kwa Wawekezaji wa Ndani na Nje, kabla ya Uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TISEZA.
Dkt. Chaya alisisitiza kuwa ORMU itaendelea kuwahakikishia wawekezaji, wafanyabiashara na wadau wote wa sekta binafsi kwamba yeye binafsi atakuwa daraja lao katika kuhakikisha malengo ya uwekezaji yanaenda sambamba na maono ya Sera na Mikakati ya Serikali.
Tukio la kihistoria la uzinduzi wa Bodi ya TISEZA na Muongozo wa Watoa Huduma limefanyika leo Jijini Dar es Salaam.
