Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA AONGOZA KIKAO CHA KWANZA CHA MAANDALIZI YA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, Januari 15, 2024 ameongoza  kikao cha kwanza cha kamati hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip, Uwanja wa Ndege Zanzibar. 

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulah ambaye ni Mwenyekiti Mwenza wa Kamati hiyo. Viongozi wengine waliohudhuria ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida pamoja na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Mipango, Bw. Lawrence Mafuru.