Habari
PROF. MKUMBO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA DENMARK NCHINI.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb,) amekutana na Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Mette Nørgaard Dissing-Spandet Machi 18, 2024 Jijini Dodoma.
Wawili hao wamejadili mambo mbalimbali ya maendeleo yakiwemo yanayohusu ushirikiano katika shughuli za Mipango na Uwekezaji kati ya Tanzania na Denmark.