Habari
PROF. MKUMBO ASHIRIKI KIKAO MAALUMU CHA MAWAZIRI WA TANZANIA NA MALAWI KATIKA SEKTA ZA UCHUMI NA UCHUKUZI

Waziri wa Nchi (OR-MU) Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.), alishiriki Kikao maalumu cha Mawaziri wa Tanzania na Malawi wanaoshughulikia Sekta za Uchumi na Uchukuzi kilichofanyika Mei 6, 2025, Jijini Dar es Salaam kujadili maeneo zaidi ya ushirikiano baina ya nchi hizo ili kuimarisha uhusiano wa uwili na kukuza diplomasia ya uchumi.