Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

Tanzania has Launches Largest Glass Factory in East and Central Africa.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan azindua kiwanda kikubwa cha cha Kutengeneza Vioo Afrika Mashariki na Kati.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Samia amesema uzinduzi wa Kiwanda hicho cha kutengeneza Vioo Barani Afrika ni ushindi mkubwa kwa Tanzania kwa kuongeza uzalishaji wa bidhaa za viwandani nchini.

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa za ajira zinazotolewa na Kiwanda cha Sapphire chenye uwezo wa kuzalisha tani 400,000 za vioo kwa mwaka na
kinatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja 1,650 na zisizo za moja kwa moja zaidi ya 6,000.

Mhe. Dkt. Samia amebainisha kuwa Kiwanda hicho kinatarajiwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini Tanzania, ikiwa ni pamoja na dolomite, mchanga wa silca, limestone, feldspar pamoja na magadi soda yanayopatikana Engaruka na kinatarajia kuuza bidhaa zake katika masoko ya ndani na nje ya nchi.