Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

TIMU YA OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI YAIBUKA KIDEDEA KATIKA MICHEZO YA SHIMIWI 2025


Timu ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji leo tarehe 2 Septemba, 2025 imeibuka kidedea katika mchezo wa Kamba (ME) kwa kuwafunga RAS Pwani kwa mivuto 2 kwa 0 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa furahisha jijini Mwanza.

Katika mchezo mwingine wa Kamba (KE), timu ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji imeiadhibu vikali timu ya RAS Pwani kwa kupata ushindi wa mivuto 2 kwa 0.

Vilevile, timu ya Mpira wa miguu ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji imetoshana nguvu na RAS Manyara kwa goli 1 - 1.

Timu ya OR - MU inatarajia kuendelea na michezo yake kesho tarehe 03 Septemba, 2025 kwa kucheza mchezo wa Kamba ME (Uwekezaji Vs Haki), mpira wa miguu ni (Uwekezaji Vs Uchukuzi) mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Sabasaba Saa nane mchana kwa upande wa mpira wa pete ni (Uwekezaji Vs GST) Saa tatu na nusu asubuhi.

Michezo ya SHIMIWI 2025 yenye lengo la kuboresha afya kwa watumishi wa Umma na kujenga mahusiano mema kazini inatarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 06 Septemba, 2025.