Habari
UAPISHO WA WAJUMBE WA TUME YA MIPANGO

Rais wa Jamhuri ya Muunagano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amemwapisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.), kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango.
Mhe. Prof. Kitila Mkumbo ameapishwa pamoja na wajumbe wenzake katika hafla fupi iliyofanyika Ikilu Chamwino Mkoani Dodoma leo Mei 29, 2024.
Wengine walioapishwa kuwa Wajumbe wa Tume ya Mipango ni Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb.), Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Ombeni Yohana Sefue, Mhe. Balozi, Dkt. Asha-Rose Migiro, Mhe. Balozi Ami Ramadhani Mpungwe na Ndg. Omar Issa.
Tume hiyo, itakuwa na lengo la kusimamia uchumi na mchakato wa upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya taifa.