Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

WAWEKEZAJI WA NDANI NA NJE KUIMARISHA UCHUMI WA NCHI


Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi M. Kida, akitoa salamu za ukaribisho na utambulisho wa wageni wakati wa Mkutano wa Waziri Prof. Kitila Mkumbo na Wawekezaji wa Ndani na Nje.

Katika salamu zake, Dkt. Kida alieleza umuhimu tukio hilo ikiwa ni pamoja kuimarisha utekelezaji wa sera na mipango ya kiuchumi inayogusa wananchi na wawekezaji wa ndani na wanaotoka nje ya nchi.

Aidha, aliongeza kuwa mwelekeo mpya wa TISEZA, utawezesha kujenga uelewa wa pamoja kwa wadau wote katika kutekeleza Dira 2050 ambayo inaakisi safari ya mabadiliko makubwa, ili ifikapo katikati ya karne ya 21 Tanzania iwe Taifa lenye ustawi, usawa na uwezo wa kujitegemea.

Mkutano huu ulitangulia uzinduzi wa Bodi mpya ya Wakurugenzi ya TISEZA na Muongozo wa Watoa Huduma kwa Wawekezaji.

Dkt. Kida amesimamia maandalizi ya tukio hili linaloonyesha azma ya Serikali ya kuboresha mazingira ya uwekezaji hususani katika kujenga Uchumi jumuishi.