Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

MASHIRIKA YA UMMA 16 KUUNGANISHWA NA MANNE KUFUTWA


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, leo Desemba 15, 2023 jijini Dar es salaam amezungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa Serikali wa kuunganisha mashirika ya umma 16 na kufuta manne kwa lengo la kuongeza tija kwa maendeleo ya nchi.

"Serikali iliunda timu ya wataalamu kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa kina kuhusu utendaji wa mashirika ya umma kwa lengo la kubainisha changamoto za kiutendaji na kupendekeza hatua za kuchukua katika kuongeza tija ya maendeleo ya nchi", ameeleza Prof. Mkumbo.

Aidha, Prof. Kitila amesema kuwa katika mchakato huo hakuna mtumishi wa umma atakayepoteza ajira na maslahi yao yatalindwa.

Kati ya mashirika na taasisi za umma zinazounganishwa ni pamoja Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini yanaunganishwa  na kuunda taasisi moja itakayohusika na utambuzi wa matukio muhimu maishani. Lengo likiwa ni kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwa na namba moja ya utambulisho.

Aidha, mashirika na taasisi za umma zilizofutwa ni pamoja na Shirika la Uzalishaji la Jeshi la Polisi na Taasisi ya Chakula na Lishe.