Habari
TANZANIA TAYARI KUVUTIA UWEKEZAJI KUTOKA JAPANI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, amesema Tanzania iko tayari kuvutia uwekezaji wa muda mrefu kuetoka Japan kwa lengo la kuongeza ajira, ujuzi, teknolojia, uzalishaji na ushindani wa bidhaa za Tanzania katika masoko ya ndani na nje.
Akizungumza katika Mkutano wa Uwekezaji na Biashara wa Tanzania uliofanyika Tokyo, Japan, Profesa Kitila amesema Tanzania inalenga kutumia nafasi yake ya kimkakati kuwa kitovu cha uzalishaji, usambazaji na biashara kuelekea masoko ya Afrika.
Amesema fursa hizo zinatokana pia na uanachama wa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Profesa Kitila amesema Serikali inalenga kuongeza angalau mara mbili uwekezaji wa Japan nchini, kutoka miradi 24 iliyosajiliwa yenye mtaji wa takribani dola milioni 42.7 za Marekani hadi kufikia miradi isiyopungua 48.
