Habari
DKT. KIDA AKUTANA NA RAIS WA SHIRIKISHO LA VIWANDA NA MAENDELEO YA UWEKEZAJI LA ALGERIA

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, amekutana na kufanya mazungumzo na Dkt. Harkati Hatem, Rais wa Shirikisho la Viwanda na Maendeleo ya Uwekezaji nchini Algeria leo Julai 13, 2024 jijini Dodoma.
Dkt. Hatem ametembelea nchini kuangazia fursa za uwekezaji katika sekta ya viwanda ambapo ameeleza nia ya kuwekeza katika sekta zifuatazo: Ujenzi wa kiwanda cha madawa na vifaa tiba, Viwanda vya kuongeza thamani ya zao la korosho, Kiwanda cha viatu, na kiwanda cha kuunganisha magari na pikipiki (automobile assembling).
Aidha, Dkt. Kida amemhakikishia Dkt. Hatem kuwa serikali inahimiza uwekezaji katika sekta anazozitafuta na kumhakikishia uwepo wa soko la ndani, Afrika Mashariki, na SADC, maeneo maalumu yaliyotengwa kwa uwekezaji, na uwepo wa malighafi zinazopatikana kwa wingi, Nguvu kazi yenye ujuzi na maarifa ya kufanya kazi za viwandani.
Vile vile, Dkt. Kida ameukaribisha uwekezaji wa Dkt. Hatem, na kwamba kwa sasa serikali imeboresha mazingira ya uwekezaji na biashara, hivyo miradi yake inauhakika wa kulindwa na kuendeshwa kwa mafanikio.