Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

Dkt. Kida akutana na Ujumbe wa Shirika la Changamoto za Milenia (MCC)


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida, amekutana na kufanya majadiliano na ujumbe wa Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), uliyoongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Tathmini (Department of Policy and Evaluation) Ndg, Nilan Fernando leo, Mei 30, jijini Dodoma.

Kikao hicho baina ya Dkt. Kida na ujumbe wake, ni mwendelezo wa vikao vya awali vya majadiliano  yanayolenga kubaini maeneo ya vipaumbele vya ushirikiano baina ya Tanzania na MCC.

Itakumbukwa kuwa, April 04, 2024, Katibu Mkuu Dkt. Kida alikutana na kufanya kikao cha aina hiyo na ujumbe wa MCC.