Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

DKT. KIDA ASHIRIKI CHA MAJADILIANO YA KUANZISHWA KWA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI NA KOREA


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida akifungua kikao kazi cha Wataalam kujadili kuhusu namna ya kuanzishwa kwa ushirikiano wa kiuchumi na nchi ya Korea.

Ufunguzi wa kikao Kazi hicho pia, ulihudhuriwa na Bw. Suleiman Mwalim Katibu Mkuu- Ofisi ya Rais Uwekezaji- Zanzibar, na Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini Bw. Togolan Mavura aliyewasilisha kuhusu nchi ya Korea na namna ambavyo nchi hizi mbili zinaweza kushirikiana kupitia Ushirikiano wa Kiuchumi.

Kikao kazi hicho kinahusisha wataalam mbalimbali kutoka kwenye Wizara na taasisi za Tanzania Bara na Zanzibar.