Habari
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akutana na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya POSCO International

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Ujumbe wake, Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya POSCO International inayowekeza kwenye Uchimbaji wa Mradi wa Madini wa Mgodi wa Mahenge Graphite ambao ni mradi mkubwa wa pili Kidunia wa Madini hayo.
Ujumbe huo Umeongozwa na Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Ghang In-Hwa. Mazungumzo hayo yamefanyika Jijini Seoul Jamhuri ya Korea tarehe 03 Juni 2024.