Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

MHE. NYONGO AWAALIKA WAWEKEZAJI KUTOKA UMOJA WA FALME ZA KIARABU (UAE) KUWEKEZA TANZANIA


Naibu Waziri wa Nchi, Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanstlaus Nyongo (Mb.) amewaalika wawekezaji kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kuwekeza Tanzania, Katika sekta za Kilimo, Madini, Utalii, Teknolojia, Mifugo na Uvuvi mifugo.

Ametoa wito huo katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji liliofanyika Dubai alipokuwa anamuwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Seleman Jafo.

Mhe. Nyongo amebainisha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini, hatua inayolenga kufungua milango ya fursa mpya za kiuchumi na kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi.

Aidha, ametoa wito kwa wawekezaji kuwa wakifikiria kuwekeza barani Afrika, wafikirie kwanza kuwekeza Tanzania.