Habari
MHE. NYONGO AWATAKA WADAU WA SEKTA YA FEDHA KUONGEZA UBUNIFU KATIKA KULETA BIDHAA BORA

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb.), ameitaka Kampuni ya Alpha Capital na wadau wengine wa sekta ya fedha kuongeza ubunifu katika kuleta bidhaa bora zaidi za uwekezaji kwenye masoko ya mitaji.
Mhe. Nyongo ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Pamoja wa Alpha Halali ambapo amesema bidhaa kama hizo zitavutia wawekezaji zaidi, hususan wale ambao hawakupata fursa za kuwekeza kutokana na imani zao.
Aidha, amewataka wawekezaji kukumbatia fursa hii ya kuwekeza katika mfuko huu ambao unalenga nchi zote za Afrika Mashariki na SADC.
"Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) ina wajibu wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kuwekeza katika mifuko ya pamoja," amsema Mhe. Nyongo.