Habari
PROF. MKUMBO AFANYA MAZUNGUMZO YA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA BALOZI WA JAMHURI YA KOREA KUSINI NCHINI TANZANIA MHE. EUNJU AHN

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Profesa Kitila Mkumbo, alifanya mazungumzo katika miadi na Balozi wa Jamhuri ya Korea Kusini nchini Tanzania, Mheshimiwa Eunju Ahn.
Mazungumzo hayo, yaliyofanyika leo, Ijumaa tarehe 28 Machi, 2025 jijini Dar es Salaam na yalilenga kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, hususani katika masuala ya uwekezaji.
Viongozi hao walijadili fursa mbalimbali za uwekezaji na njia za kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kwa manufaa ya mataifa yote mawili.