Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

PROF. MKUMBO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MENEJA WA KAMPUNI YA UTAFITI WA MAFUTA NA GESI YA EQUINOR


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.), leo tarehe 6 Novemba, 2024 jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Meneja mpya wa kampuni ya utafiti wa mafuta na gesi Equinor-Tanzania, Bi. Hilde Merete Nafstad, aliyefika ofisini hapo kwa lengo la kujitambulisha.

Mhe. Prof. Mkumbo amemhakikishia Bi. Hilde Merete Nafstad ushirikiano kutoka Serikalini katika Utekelezaji wa shughuli zake hapa nchini.