Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

PROF. MKUMBO APOKEA TAARIFA YA MAPITIO YA RASIMU YA DIRA 2050


Mhe. Profesa Kitila Mkumbo (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, amepokea Taarifa ya Mapitio ya Rasimu ya Dira 2050 kutoka kwa wajumbe wa timu ya mapitio ya rasimu hiyo.

Kikao hicho muhimu baina ya Mhe. Prof. Mkumbo na Timu ya Mapitio ya Rasmu ya Dira 2050, kilichohudhuriwa na Katibu Mkuu Dkt. Tausi Kida Mbaga, kimelenga kuboresha rasimu ya Dira 2050 kupitia mapendekezo ya timu hiyo.

Aidha, timu ya mapitio ya rasimu ya Dira 2050 imezingatia ushirikishwaji mpana wa wadau kutoka sekta za umma, binafsi na asasi za kiraia.

Baada ya kupokea taarifa ya mapitio, Mheshimiwa Waziri Prof. Mkumbo amewashukuru wajumbe wa timu ya mapitio kwa kazi kubwa waliyoifanya na kuiagiza timu kuu ya uandishi wa Dira kuzingatia mapendekezo yote yaliyotolewa na kuchukua hatua zinazofaa kuzalisha rasimu ya Dira 2050 yenye viwango vya juu vya ubora.

Vile vile, Mheshimiwa Prof. Mkumbo amewasihi wajumbe wa timu ya Mapitio ya Rasimu ya Dira 2050 kuendelea kutoa ushirikiano kwa Timu Kuu ya Uandishi wa Dira 2050 ili kutoa ufafanuzi zaidi juu ya mapendekezo waliyotoa.