Habari
PROF. MKUMBO ASHIRIKI MKUTANO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUJADILI MASUALA MUHIMU YA KIKANDA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb), pamoja na Katibu Mkuu Dkt. Tausi Kida, wameungana na ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kujadili masuala muhimu ya kikanda.
Kikao cha viongozi hao kimelenga kupokea taarifa muhimu kuelekea Mkutano wa 46 wa Baraza la Mawaziri wa EAC unaotarajiwa kufanyika leo Novemba 28.
Itakumbukwa kuwa kikao hiki kinachofanyika Jijini Arusha ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa 24 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa EAC utakaofanyika tarehe 29 na 30 Novemba, 2024.
Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi unatarajia kujadili hatua za kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kuhakikisha maslahi ya wananchi wa Afrika Mashariki yanazingatiwa.