Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

SERIKALI KUJENGA MAENDELEO YENYE HAKI NA USAWA - PROF. MKUMBO


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb), amesema Serikali itaendelea kusimamia haki, usawa na uwajibikaji kama nguzo kuu za maendeleo.

Akifungua kikao cha kimkakati na wadau wa haki za binadamu leo Aprili 08, 2025 Jijini Dodoma, Prof. Mkumbo amesema hakuna maendeleo bila haki, na hakuna haki bila usawa wa fursa. 

Aidha, amebainisha kuwa Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo unalenga kuongeza wilaya zenye watoa msaada wa kisheria kutoka 52 hadi 138 mwaka huu.

Vile vile, alitumia fursa hiyo kuto kutoa pongezi kwa mashirika kama THRDC, TLS, ZLS na East Africa Law Society kwa mchango wao katika utetezi wa haki na majadiliano ya kisheria. 

Aidha, amesema ushirikiano kati ya Serikali na mashirika hayo ni utekelezaji wa Mpango wa Taifa na Sheria ya Tume ya Mipango ya 2023.

“Majadiliano haya ni chachu ya sera jumuishi na maendeleo yanayoendana na hali halisi ya jamii,” alisisitiza.