Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

SERIKALI NA WAZALISHAJI WA SUKARI NCHINI WAMEKUTANA NA KUKUBALIANA KUSHIRIKIANA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOKABILI SEKTA HIYO.


Serikali na wazalishaji wa sukari nchini wamekutana na kukubaliana kushirikiana kutatua changamoto zinazokabili sekta hiyo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.), akiambatana na Katibu Mkuu, Dkt. Tausi Kida alikutana na wawekezaji katika sekta ya uzalishaji wa sukari na kuwahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Sita imechukua hatua za kuboresha mazingira ya uwekezaji, ikiwa ni pamoja na viwanda vya sukari. 

Aidha, alisema kuwa mabadiliko yoyote ya sera na sheria yana lengo la kuboresha mazingira na kulinda watumiaji.

Serikali na wawekezaji wamekubaliana kushirikiana katika maeneo sita muhimu, ikiwa ni pamoja kuangalia uwezekano wa kufanya mapitio ya Sheria ya Sukari ili ikidhi mahitaji ya wakati.