Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

TUMEFANIKIWA KUTUNZA UHALALI WA UWEPO WA WIZARA - MHE. PROF. MKUMBO


Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji imetimiza Mwaka mmoja kwa kuzindua Taarifa za Maboresho ya Mazingira ya Uwekezaji na Biashara na Nyenzo za Usimamizi wa Uwekezaji Nchini.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, amesema kuwa ndani ya Mwaka huo Ofisi imejijengea uhalali wa kuendelea kuwepo.

"Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita tumetekeleza majukumu yetu vyema na ninaweza kusema bila kigugumizi kuwa tumeweza kumthibitishia Mhe. Rais kuwa uamuzi wake wa kuunda ofisi hii ulikuwa sahihi" amesema Mhe. Prof. Mkumbo.

Aidha, Mhe. Prof.  Mkumbo amesema kuwa Ofisi imefanya mambo mengi katika kipindi cha muda mfupi ambayo yamejenga uhalali wa uwepo wa Ofisi hiyo kuwa muhimu.

"yapo mengi ya msingi tuliyoyafanya na tunaendelea kuyafanya kwa mafanikio kwa mfano tumeendelea kusimamia vyema mchakato wa kuandika Dira ya taifa 2050 kwa kiwango ambacho watanzania waliowengi mchakato huu wanaujua, wanaufuatilia na kwa kweli walio wengi wameshiriki kutoa maoni" amesema

Aidha, amesema kuwa Ofisi hiyo imeweza kusimamia vyema taasisi ambazo Mhe. Rais alitukabidhi tuzisimamie ikiwemo Ofisi ya Msajili wa Hazina, Tume ya Mipango, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na EPZA."

Leo pia tupo hapa kuzindua baadhi ya matokeo ya kazi tulizozifanya katika kipindi cha mwaka mmoja tangu Mhe. Rais aunde ofisi hii. Mhe Waziri Mkuu moja ya jukumu la Msingi la wizara za kiserikali ni kuanzisha michakato ya kutunga sheria na sera.

Prof. Mkumbo ameongeza kuwa nyaraka zitakazoenda kuzinduliwa ni pamoja na Taarifa ya Tathimini ya Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji Nchini, Taarifa ya Uwekezaji ya Kitaifa 2023, Tafiti ya awali kuhusu maeneo maalumu ya kiuchumi, Mwongozo wa Uendelezaji na usimamizi wa maeneo maalumu ya kiuchumi (SEZ), Mifumo ya Kieletroniki ya kuhudumia wawekezaji wa EPZA na Mpango Mkakati wa Mpito wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji.