Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji

Habari

WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA AONGOZA KIKAO CHA TIMU YA KITAIFA YA DIRA


Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), ameongoza kikao maalum cha timu ya Kitaifa ya Dira kilichofanyika leo Novemba 29, Zanzibar.

Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi mabalimbali, akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, pamoja na viongozi waandamizi kutoka pande zote mbili za Muungano.

Kwa upande wa Tanzania Bara, walikuwepo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb), Naibu Waziri Mhe. Stanslaus Nyongo (Mb), na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Tausi Kida.

Kutoka Zanzibar, Waziri wa Nchi, Afisi ya Rais (Fedha na Mipango), Mhe. Dr. Saada M. Salum, aliongoza ujumbe wa viongozi wengine wa ngazi za juu.